Psalms 54

Kuomba Ulinzi Wa Mungu Kutokana Na Adui

(Kwa Mwimbishaji: Na Ala Za Nyuzi Za Uimbaji. Utenzi Wa Daudi. Wakati Mtu Mmoja Wa Zifu Alipomwendea Sauli Na Kumjulisha Kuwa Daudi Amejificha Kwao)


1 aEe Mungu uniokoe kwa jina lako,
unifanyie hukumu kwa uwezo wako.

2 bEe Mungu, sikia maombi yangu,
usikilize maneno ya kinywa changu.


3 cWageni wananishambulia,
watu wakatili wanayatafuta maisha yangu,
watu wasiomjali Mungu.


4 dHakika Mungu ni msaada wangu,
Bwana ndiye anayenitegemeza.


5 eMabaya na yawarudie wale wanaonisingizia,
kwa uaminifu wako uwaangamize.


6 fNitakutolea dhabihu za hiari;
Ee Bwana, nitalisifu jina lako
kwa kuwa ni vyema.

7 Kwa maana ameniokoa katika shida zangu zote,
na macho yangu yamewatazama adui zangu kwa ushindi.
Copyright information for SwhKC